Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans van Der Pluijm ameipa mtihani mkubwa Young Africans kwenye Michuano ya Kimataifa, baada ya kupangwa kwa Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika jana Jumanne (Agosti 09), mjini Cairo-Misri.

Young Africans imepangwa kucheza dhidi ya Mabingwa wa Soka wa Sudan Kusini Zalan FC, ambao wataanzia nyumbani, kabla ya kumalizia Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha huyo kutoka nchini Uholanzi ambaye pia aliwahi kukinoa kikosi cha Young Africans amesema ikitokea klabu hiyo ikaondoshwa kwenye hatua ya awali atashangaa sana, kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa klabuni hapo.

Amesema Young Africans imefanya usajili mkubwa ambao unaakisi michuano ya Kimataifa, hivyo ni wajibu kwao kuhakikisha wanapambana na kuvuka hatua hiyo ya awali.

“Kwa Uwekezaji na Usajili waliofanya Young Africans Msimu huu wakitolewa hatua za awali Klabu Bingwa Afrika nitawashangaa sana,”

“Nafikiri hiki ndio kipindi Vilabu vyetu vinapaswa kupambana kufanya vizuri Kimataifa.” amesema Kocha Hans

Endapo Young Africans itavuka katika hatua ya awali dhidi ya Zalan FC, itakutana na Mshindi wa kati ya St. George dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Mama kizimbani kwa mauaji ya kimada wa mumewe
Waziri Mkuu: Mkutano Mkuu CAF utafungua njia kimataifa