Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kufanya majaribio ya makombora mapya ya masafa marefu .

Aidha hayo ndiyo majaribio ya kwanza ya kufanywa na taifa hilo katika kipindi cha miezi kadhaa na yanaonesha jinsi nchi hiyo inavyozidi kupanua uwezo wake wa kijeshi wakati kuna malumbano ya nyuklia kati yake na Marekani.

Kituo kikuu cha habari cha Korea kimesema leo septemba 13, kuwa makombora hayo ambayo yalikuwa yanaundwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, yamekwenda umbali wa kilomita 1,500 kilomita (930miles) wakati wa majaribio.

Nchi hiyo imeyasifu makombora hayo ikisema ni zana zenye umuhimu mkubwa ambazo zinaafiki wito wa kiongozi Kim Jong Un wa kuliongezea nguvu jeshi la nchi hiyo.

Jeshi la Korea Kaskazini halijathibitisha moja kwa moja majaribio hayo.

Barbara aishauri Young Africans
Rais Samia atoa agizo kwa wakuu wa mikoa