Daktari bingwa wa afya ya Akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Doroth Mushi ku amefafanua juu ya tatizo linalowapata watoto wengi na vijana la kukojoa kitandani, amesema kuwa kutokwa na haja ndogo kitandani si hali ya kawaida bali ni tatizo liliopo katika kundi la magonjwa ya akili.

Amesema kuwa watu wengi hawajui kwamba hadi mtu kujikojolea kitandani ni tatizo lilipo kwenye mfumo wa fahamu kukosa mawasiliano mazuri.

‘Hali hiyo hupelekea mtu kushindwa kuhimili hali ya kujizuia haja ndogo akiwa usingzini ‘ Amesema Doroth Mushi.

Hivyo amepinga vikali tabia ambayo wazazi na walezi hufanya ya kuwaadhibu watoto au vijana wenye shida hiyo kwani ni wakati sasa watambue kuwa si makusudi bali ni ugonjwa.

‘Wazazi na walezi wengi kwa kuwa hawajui ni ugonjwa wanishia kuwapiga watoto na kuwatembeza mtaani wakidhani kuwa ni adhabu kumbe wanaongeza tatizo juu ya tatizo’’ ameseam Dk. Doroth Mushi.

Pia ameeleza ndoa  nyingi huvunjika kwa sababu ya tatizo hilo kwa kukosa maelewano baina ya wanandoa hao.

Ametaja moja ya sababu inayopelekea tatizo hilo ni mama akipata uchungu muda mrefu hufanya motto kukosa hewa  ya kutosha ya oksijeni kwenye ubongo wake hivyo ni ni hatari kwa mtoto kwani baadae husababisha kupata magonjwa ya akili.

Daktari ameshauri kuwa wazazi na walezi  wanaolea vijana na watoto wenye shida hiyo kuacha kuwaficha watoto wenye shida hiyo  badala yake wawapeleke hospitali.

Mbowe aelezea maendeleo ya hali ya Tundu Lissu
Video: Chadema kuchangia damu nchi nzima

Comments

comments