Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa leo ameingia ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu alipoingia Bungeni humo kwa mara ya mwisho akiwa mbunge.

Lowassa ambaye alikuwa mjini Dodoma siku mbili kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge, aliingia bungeni humo leo majira ya saa 2 asubuhi na kusalimiana na wabunge pamoja na viongozi wengine wa CCM na Ukawa kabla ya kukaa katika sehemu maalum ya wageni na kufuatilia kikao cha Bunge.

Viongozi mbalimbali wa Ukawa walikutana na wabunge wa umoja huo mjini Dodoma kwa kile walichodai kuweka mkakati wa pamoja wa namna ya kukabiliana na hoja za Serikali ikiwa ni pamoja na kupinga muswada wa Sheria ya huduma za habari usisomwe.

Mwanasiasa huyo mkongwe alikuwa Mbunge wa Monduli hadi mwaka 2015 alipoamua kung’atuka na kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais.

Lukaku Awapotezea Viongozi Wa Everton
ZIFA Waialika Taifa Stars Mjini Harare