Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa, amesema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ina watu wenye roho mbaya kwani waliwahi kumuombea kifo,lakini hadi leo anadunda.

Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), amesema baadhi ya waliomwombea kifo leo hawapo duniani,kwani mungu ndiye anayepanga maisha ya mwanadamu.

“Kule kwa wenzetu kuna watu wenye roho mbaya,kwani hata mimi waliniombea kifo,waliniombea kifo muda mrefu kweli lakini mpaka sasa bado nadunda tu wakati baadhi ya walioniombea hivyo,leo hawapo duniani kwa mapenzi ya mungu”amesema Lowassa.

Aidha, Lowassa ameyasema hayo baada ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa ufunguzi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Matevezi jimbo la Arumeru Magharibi,kupaza sauti wakimuuliza juu ya hatima ya mbunge wao Lemaambaye yupo Gereza la kisongo kwa miezi miwili sasa.

Hata hivyo, Lowassa amemnadi mgombea wa Chadema,Abel Jeremiah amewataka timu ya kampeni na wananchi kuhakikisha kura haziibiwi kwa kile alichoeleza kuwa Chadema ina nguvu.

Bisimba: Serikali chanzo cha migogoro ya ardhi
Rooney afunguka ya moyoni baada ya kuifikia rekodi ya magoli ya Charlton

Comments

comments