Wasanii wa Bongo Movies, Single Mtambalike maarufu kama Richie na Elizabeth Michael maarufu kama Lulu waliing’arisha Tanzania kwenye tuzo kubwa za filamu za African Magic Viewers Choice Awards (VMAs), zilizotolewa wikendi iliyopita jijini Lagos, Nigeria.

Wasanii hao walifanikiwa kushinda tuzo moja moja na kupenya msitu wa waigizaji wengine wakubwa Afrika. Richie alishinda tuzo ya Filamu ya Kiswahili (Best Indigenous Language Movies/TV Series – Swahili), kwa filamu yake ya Kitendawili.

Richie aliwashukuru mashabiki wake na kueleza kwa lugha ya kiingereza, “asanteni kwa kuliita koleo… kole, na sio kijiko kikubwa, asanteni sana.”

lulu (1)

Kadhalika, Lulu alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya filamu bora Afrika Mashariki (Best Movie – East Africa) kupitia ‘Mapenzi’.

Lulu alionesha furaha ya aina yake na kububujikwa na machozi wakati akiwashukuru mashabiki wake baada ya kupokea tuzo hiyo ambayo aliitaja kama ndoto yake tangu alipoingia kwenye tasnia ya uigizaji akiwa na umri wa miaka mitano.

“Kwanza kabisa ningependa kumshukuru Mungu wangu wa ajabu. Ningependa pia kuishukuru familia yangu hasa mama yangu, imekuwa ni safari ndefu tangu nikiwa na miaka mitano mpaka leo lakini siku zote wamekuwa wakiniunga mkono. Ningependa kumshukuru kila mtu aliyeshiriki kwenye filamu hii. Siwezi kuwataja wote lakini asanteni sana. Na mwisho… Ohh my God, mashabiki wangu wapendwa, ninyi ni mnashangaza, mmefanya hili liwezekane. Tangu nikiwa na miaka mitano nilikuwa nikiota hili, mmelifanikisha, asanteni sana.”

Swaiba wa Lulu, Ali Kiba alikuwa miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva waliohudhuria tukio hilo na alitumbuiza wimbo wake wa ‘Mwana’.

Ali Kiba

Ofisi za CUF zachomwa moto Zanzibar
Unyama: Mwanafunzi abakwa na kuuawa kikatili