Wakati Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’ likiendelea na mpango wa kutoruhusu mashabiki kuingia katika baadhi ya vuiwanja vinavyotumika kwa ajili ya Michuano ya Vilabu Barani humo, Uongozi wa Azam FC umetangaza kufunga Luninga Kubwa nje ya Uwanja wa Azam Complex Chamazi ili kuwapa fursa Mashabiki wao kushuhudia mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho Mzunguuko wa Kwanza.

Azam FC itakua wenyeji wa Pyramids FC ya Misri Jumamosi (Oktoba 16), katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, huku lengo kubwa kwa klabu hiyo ni kusaka ushindi utakaowaweka katika mazingira mazuri kabla ya mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa nchini Misri Mwishoni mwa juma lijalo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao za klabu hiyo, Uongozi wa Azam FC umeona njia ya kufunga Luninga kubwa nje ya Uwanja wa Azam Complex Chamazi, itatoa fursa kwa Mashabiki wao kujihisi wako na timu yao Uwanjani.

Kikosi cha Pyramids Fc kinatarajiwa kuwasili Jijini Dar es salaam leo Jumatano (Oktoba 13) majira ya usiku, tayari kwa mchezo huo.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho ‘CAF’ utakuwa wa pili kwa Azam FC, baada ya kuing’oa Horseed FC ya Somalia jumla ya mabao 4-1, huku Pyramids FC utakua mchezo wao wa kwanza msimu huu, kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’.

Mr Tanzania kutafutwa Octoba 22, 2021
Rais Samia Kinara kuhakikisha wanawake hawaachwi nyuma kiuchumi: Dkt.Gwajima