Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesema maadhimisho ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka oktoba 11, yakiwa na lengo la kuitikia azimio la umoja wa mataifa la kuwalinda watoto wa kike, mwaka huu yatafanyika mkoani shinyanga yakiwa na lengo la kuelimisha na kuhamasisha  jamii kutambua umuhimu wa kutetea haki za watoto wa kike na kutoa fursa ya kutathmini changamoto zinazowakabili watoto hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto Bi. Margaret S Mussat alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, alisema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ”Mimba na Ndoa za Utotoni Zinaepukika:Chukua hatua kumlinda mtoto wa kike” hii ni kwaajili ya kuwakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto hawaolewi katika umri mdogo.

Bi. Margaret  aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo wasichana wapatao milioni moja wanatarajiwa kuwa wameolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18 duniani kote, na  katika bara la afrika asilimia 42 ya wasichana wote  huolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Aidha Takwimu kutoka Ofisi ya  Taifa  zinaonyesha  kuwa mkoa unaoongoza kwa kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni  hapa nchini ni Shinyanga amabayo ina asilimia 59, Tabora 58%, Mara 55%, Dodoma 51%, Lindi 48%, Mbeya 45%, Morogoro42%, Singida 42%, Rukwa 40%, Ruvuma 39%,Mwanza 37%, Kagera 36%, Mtwara 35%, Manyara 34%, Pwani 33%, Tanga 29%, Arusha 27%, Kilimanjaro 27%, Kigoma 29%, Dar es salaam 19% na Iringa yenye asilimia nane.

Hata hivyo Bi. Margaret amesema  serikali inaendelea  kuwaelimisha   wazazi na walezi kutambua athari zinazotokana na uwepo  wa ndoa za utotoni ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili, hivyo maadhimisho hayo yatatumika kuelimisha wazazi na walezi na jamii kutambua kuwa kumuozesha mtoto  katika umri chini ya miaka 18 ni kumuathiri   kimwili na kingono.

Uamuzi Wa Kamati Ya Bodi Ya Uendeshaji Ligi
Xavi Abadili Kauli Dhidi Ya Cristiano Ronaldo