Maaskofu wasaidizi jimbo la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini na Mshashamu Eusebius Nzigilwa wa jimbo kuu katoliki la Dar es salaam wametoa taaarifa kuwa wameamua kurudisha mgao wa fedha za Escrow ambazo walipewa na James Rugemalira.

Viongozi hao wa dini wamesema wameamua kurudisha fedha hizo za serikali kutokana na kuwepo kwa kesi mahakamani ya kuhujumu uchumi inayomkabili James Rugemalira ambaye ndiye aliwapa fedha hizo.

Mhashamu Method Kilaini alidaiwa kupewa jumla ya fedha za kitanzania milioni 80.5 huku Eusebius Nzigilwa akidaiwa kupewa jumla ya milioni 40.4 ambazo zote kwa ujumla wamesema wanarudisha fedha hizo Serikalini.

Macron: Ulaya inahitaji mijadala, vinginevyo itakufa
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 8, 2017