Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015, Laurence Mabawa, ameahidi kutumia gharama zake kuzunguka nchi nzima kueneza kampeni ya ‘Magufuli Baki’.

‘Magufuli Baki’ ni kampeni maalumu ya kumtia moyo Rais Magufuli kwa kile anachokifanya cha kutetea haki za wanyonge, hivyo lengo kuu ni kumwomba Rais abaki katika  msimamo wake wa kutetea maskini.

”Napinga kwa nguvu zangu zote, kama nilivyokwisha fafanua toka mwanzo, Kampeni ya ‘Magufuli Baki’ ina lengo la kumtia moyo Magufuli na kumwomba abaki katika msimamo wake wa kutetea maskini, wanyonge na kupigania rasilimali zetu”, amesema Mabawa.

Mabawa amesema, atatumua gharama zake kuzunguka nchi nzima na kuhamasisha wananchi kutoa maoni yao juu ya Rais kuendeleza msimamo wake wa kiutendaji na kuteta haki za wanyonge.

”Nirudie tena wito wangu kwamba nitazunguka nchi nzima kwa gharama zangu kupata fursa ya kuwasikiliza wanamchi wakitoa maoni juu ya Rais kuendeleza msimamo wake wa kiutendaji”. amesema Mabawa.

Aidha ameeleza kutorudishwa nyuma na propaganda za baadhi ya watu wataomkejeli kwa kile ambacho ameamua kukifanya ‘Magufuli Baki’.

Pamoja na hayo amedai kwamba toka aitangaze kampeni yake kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao hutoa lugha za maudhi na kejeli kwa baadhi ya Watanzania wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

Video: Bi Hindu afyatuka, asema Klabu ya Simba haihitaji mabadiliko
Majaliwa: Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji nchini