Wanananchi wameshauriwa kulinda na kufanya matumizi sahihi ya umeme wawapo majumbani ili kuepukana na ajali za moto hasa ule unaoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari leo meneja wa afya na usalama kazini Eng. Majige J Mabula amesema kuwa ajali za moto zinavyoanza huanza kama moto wa viberiti au vyanzo vya viwashio vingine hivyo ni vema kuepuka kuweka vitu vinavyoshika moto kiurahisi karibu na nyaya au maungio ya nyaya za umeme ndani ya nyumba kama magodoro, vyandarua na vingine vingi

Eng. Mabula amewashauri wananchi kuwa makini katika matumizi bora ya vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi, hita za umeme kompyuta pamoja na vifaa vingne vya umeme kwa kuvizima na kuvitoa kwenye umeme baada ya matumizi.

Aidha Bw. Mabula amewashauri watumiaji wa umeme kutoa taarifa TANESCO pindi mtumiaji anapotaka kuongeza matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa ndani ya makazi  ili waweze kutathmini uwezo wa nyaya kukidhi mahitaji na kuepusha milipiko ya moto.

Hata hivyo amesisitiza kwamba wakandarasi wana uwezo mkubwa wa kuzuia ajali za moto pale wanapokuwa wakifanya shughuli za ujenzi kwa kuzingatia rangi za kuta, milango imara na hata ujenzi wa madirisha  ili kuzuia moto usisambae  ndani ya nyumba.

Video: Mbunge Ally Kessy Aguswa na Haya Bungeni, Aachia Ujumbe Kwa 'Style', Tazama
Rais Magufuli amteua Mizengo Pinda kushika nafasi hii

Comments

comments