Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewapunguzia adhabu wafungwa   256 waliohukumiwa kunyongwa kwa kuwabadilishia hukumu na kusema sasa wapewe kifungo cha maisha.

Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo Desemba 9,2020 ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika,  wakati alipokuwa akitoa hotuba baada ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri aliowateua Desemba 5,2020.

 “Kuna Wafungwa 3316 wana makosa madogo hawa nawapunguzia adhabu na wengine waachiwe, tangu 2015 nilitakiwa niwe nimewanyonga Wafungwa 256, sijanyonga hata mmoja na hao 256 nawapunguzia kifungo chao cha kunyongwa sasa wafungwe maisha” amesema Rais Magufuli.

“Kama atakayekuja atawanyonga Wafungwa sawa lakini Mimi nasita yaani ninyonge Wafungwa 256 wakati wao wameua watu wawili, si bora ninyongwe mimi hapohapo bila kupelekwa mahakamani” ameongeza Rais magufuli.

Kigwangala awajibu wanaomsakama Mitandaoni
Magufuli amtaka Jafo kumtumbua Mkurugenzi Geita