Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka wakuu wa mikoa, wilaya, na wakurugenzi wa halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye mazao ili wakulima wanufaike kutokana na kujiongezea kipato.

Ametoa agizo hilo wakati akihutubia wakazi wa Bukoba na watanzania kwa ujumla akiwa katiaka ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kagera.

“Nawaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri, kupitia upya kodi zilizopo katika bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba. hakikisheni mnaondoa utititri huu wa kodi ili wafanya biashara hawa wafaidike na mazao yao”amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali iytikadi za dini na kabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika nyanja zote za kimaendeleo.

Muhongo atoa siku 15 kwa mkandarasi kuunganisha umeme
Majaliwa atoa onyo kali kwa wanaokata miti