Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, dkt. John Magufuli amesema tayari ameongea na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa njia ya simu na kumaliza mgogoro uliopo kwenye mipaka ya nchi hizo kutokana na virusi vya Corona.

Amebainisha hayo leo Mei 20 Mjini Singida alipokuwa safarini akirejea Dodoma kutoka Chato na kusisitiza kuwa mgogoro huo ni mdogo hawezi kukubali ukwamishe shughuli za biashara baina ya nchi hizo mbili.

Magufuli amesema wamewaachia mawaziri wa uchukuzi wa nchi zote mbili pamoja na wakuu wa mikoa ali kupata njia nzuri kwa maslahi mapana ya nchi zote kwani huu ni wakati wa kujenga uchumi haitakiwi kushindwa kufanya biashara kwa kisingizio cha Corona.

“Tumezungumza vizuri na mheshimiwa Kenyatta, sisi tumeyamaliza, wakae viongozi watatue hili tatizo na watu wafanye biashara katika pande zote mbili…nataka wakenya na watanzania wafanye biashara yao vizuri” amesema Magufuli.

Aidha amebainisha kutokubaliana na taarifa kuwa idadi kubwa ya madereva kutoka Tanzania wanakutwa na corona nchini Kenya “Haiwezekani kila dereva anayekwenda huko awe na korona” na kutoa rai kuwa cocora isije ikagombanisha nchi hizo.

Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Tanga ni mikoa ambayo inamipaka inayounganisha nchi ya Kenya na Tanzania

Bigirimana aipa masharti Young Africans
Dilunga kubaki Simba SC kwa miaka miwili