Rais John Magufuli amesema kuwa ataendelea kuwatumikia wananchi na kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa kujitoa sadaka kwani anaamini kazi hiyo amepewa na Mungu kwa ajili ya kuwatumikia watu wa Mungu.

Dk. Magufuli amesema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano wa makandarasi jijini Dar es Salaam ambapo aliandamana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alisisitiza kuwa hatavumilia vitendo vya rushwa na ufisadi na kwamba ni bora asiwe Rais kuliko kuwa na uvumilivu katika uozo huo.

“Ni mara 10 nisiwe Rais, nikachunge hata ndege, nikakae kijijini kuliko niwe Rais halafu nivumilie uozo huu unaofanyika. I’m saying never,” alisema Rais Magufuli.

“Kama ni kutumbua kila siku nitatumbua tu. Watu lazima wabadilike. That is my direction and I will never change,” aliongeza.

Aliwataka Makandarasi kuhakikisha wanakuwa na uzalendo wanapofanya kazi na Serikali kwa kutopandisha gharama za zabuni kwa lengo la kuweka asilimia kadhaa za kuwalipa watendaji wa Serikali.

Alisema kuwa kama wazabuni hao wanapandisha bei kwa lengo la kuwapa asilimia kadhaa watendaji hao, waripoti vitendo hivyo Takukuru.

“Kama hiyondiyo sababu, tuna chombo chetu cha Takukuru. Kwanini hamkitumii? Kwanani mnakubaliana na wale wanaowaomba rushwa? Kwanaini kila mahali mnapoomba zabuni unaweka aslimia ya kulipa rushwa? Rais Magufuli alihoji.

Alisema kuwa endapo watashirikiana na Serikali na kupelekea baadhi ya watendaji kufungwa kwa makosa ya kupokea rushwa, gharama za miradi zitashuka.

Video: Trilion 1.3 zilizoombwa na Wizara ya Elimu na Mgawanyo Wake
VIDEO: MAGAZETI LEO 27 MAY 2016

Comments

comments