Mtendaji mkuu wa klabu ya Inter Milan, Piero Ausilio, ameripotiwa kutua jijini London kwa lengo la kukamilisha mazungumzo ya kuuzwa kwa mlinda mlango wa klabu hiyo Samir Handanovic.

Klabu za Arsenal na Chelsea zinatajwa kuwa katika purukushani za kumuwania mlanda mlango huyo kutoka nchini Slovenia, na zote zipo tayari kutoa ofa nzuri kwa ajili ya kumsajili.

The Gunners wamepanga kuongeza ushindani katika nafasi ya mlinda mlango kwa kuamini endapo watafanikiwa kumsajili Handanovic, kutakua na upinzani wa kweli dhidi ya mlinda mlango wao namba moja kwa sasa Pete Cech.

Samir Handanovic

Chelsea wao wanahitaji saini ya Handanovic, kama silaha ya kujihami na mpango wa kuwa katika hatari ya kumpoteza mlinda mlango wao namba moja Thibaut Courtois, alietishia kuondoka klabuni hapo, huku klabu ya Real Madrid ikiweka mikakati ya kumsajili.

Inter Milan tayari wameshatangaza nia ya dhati ya kumuweka sokoni Handanovic mwenye umri wa miaka 31, kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 12 hadi 15.

Mazzarri Kuanza Na Usajili Wa Oscar Hiljemark
Adui Wa Liverpool Kujisogeza Nyumba Ya Jirani

Comments

comments