Mahakama kuu kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi yaliyompa ubunge Onesmo Nangole wa chadema kutokana na udanganyifu
Jaji anayesikiliza kesi hiyo Sivangilwa Mwangesi amesema ni kutokana na udanganyifu ambapo fomu zilitomika kuandika matokeo ni fomu 21b za udiwani badala ya kutumia fomu 21c ya ubunge  hivyo uchaguzi utarudiwa
Katika shauri hilo aliyekuwa Mgombea ubunge wa ccm jimbo la longido Dr Steven Kiruswa alipeleka shauri hilo mahakamani dhidi ya mbunge aliyekuwa mbunge wa longido Onesmo ole Nangole
Bw. Nangole ambaye ametenguliwa ubunge leo hii aliwahi kuwa Mwenyekiti wa ccm mkoa wa arusha kabla ya kuhamia chadema agosti 8 2015 .