Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, jana ilitoa uamuzi wa kufuta kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali iliyokuwa ikiwakabili viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa wilaya hiyo.

Viongozi hao ni pamoja na Katibu wa chama hicho ngazi ya wilaya, Emmanuel Nabora, diwani wa kata ya Ndumet, Jackson Rabo na diwani wa viti maalum, Witness Nerey.

Katika kesi hiyo namba 86 ya mwaka 2016 iliyosikilizwa na Hakimu Mkuu Mkazi, Arnold Kirekiano, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili.

Ilielezwa kua katika kosa la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usioruhusiwa kisheria Agosti 24 majira ya saa nne na nusu asubuhi katika eneo la Sanya Juu wilayani Siha.

Hata hivyo, kesi hiyo ilifutwa na washtakiwa wote wako huru.

Mpina awataka wawekezaji kuwa wabunifu katika utunzaji mazingira
Real Madrid Wapunguziwa Mzigo Wa Adhabu