Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefuta posho zote zinazotolewa katika vikao vinavyoitishwa katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam.

Aidha, Majaliwa ametoa siku tatu kwa watumishi 10, ambao walitakiwa kuhamia Wilaya ya Kigamboni lakini bado wanaendelea kuwa Wilaya ya Temeke kuripoti mara moja.

Hatua hiyo imetokana na ombi lililotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Ally Hapi ambapo aliiomba Serikali kufuta posho hizo na fedha zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo.

“Mkurugenzi ukiruhusu hili liendelee unajipa nafasi ya wewe kutokuwepo katika nafasi yako, naomba hili lisitokee tena,”amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amewataka watumishi wa Halmashauri ya Kigamboni kufanya kazi kwa bidii na kufuata maelekezo ya Rais Magufuli.

UVCCM waunga mkono kutumbuliwa kwa Mramba
Utumbuaji majipu wageukia mahakimu