Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku kuweka bei ya tumbaku kwa dola za Marekani badala yake inunuliwe kwa shilingi za Kitanzania, sababu imechangia kuwaumiza wakulima wa zao hilo.

Amesema kuwa wanunuzi wa zao hilo wana uhuru wa kuweka bei zao kwa dola lakini bei hiyo itafsiriwe kwa shilingi za Kitanzania ili wakulima waweze kutambua bei elekezi tangu mwanzo wa msimu.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika mkoani Tabora.

“Kwa mfano, mkulima anapouza tumbaku anaambiwa kilo zake zina thamani ya dola za marekani 90. Wakati anapokuja kulipwa bei ya shilingi inakuwa imebadilika, kwa hiyo kama aliuziwa wakati thamani ya dola moja ikiwa ni sh. 1,500/- na wakati wa kulipwa imefikia sh. 2,000/- hatalipwa kwa bei ya sasa. Bali atalipwa kwa bei ileile ya zamani jambo ambalo linamuumiza mkulima,” amesema Majaliwa

Hata hivyo, Majaliwa ambaye katika ziara yake mkoani Tabora, ameonya juu ya mkanganyiko unaowapata wakulima na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) kwenye kutafsiri bei ya zao hilo kutoka dola za Marekani.

 

Liverpool FC Yaikatalia FC Barcelona
Mfumuko wa bei nchini wazidi kushuka