Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), wametakiwa kuendelea kutafuta vyanzi vipya vya maji na kuviingiza kwenye mfumo wa uzalishaji na usambazaji maji.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Novemba 29, 2022 alipotembelea mradi wa maji Kisarawe mjini, mkoani Pwani.

Amesema kuwa licha ya kuongezeka kwa kiwango cha maji kwenye mfumo wa uzalishaji na usambazaji, wasilale bali waendelee kuwatumia wataalam wa ndani kutafuta maji zaidi.

Majaliwa ameongeza kuwa, kumekuwa na ongezeko la makazi, viwanda na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji uwepo wa maji ya kutosha.

“Tusilale tuendelee na uzalishaji wa maji, Tunataka huduma hii isambae na iwafikie watu wote” amesema Majaliwa.

“Ndugu wafanyakazi wa DAWASA mnapaswa kutambua maji ni huduma nyeti kwenye maisha ya binadamu, kazi yenu inahitaji uaminifu na uadilifu mkubwa, fanyeni kazi hii ya umma, wahudumieni watanzania, tambueni maeneo yenye uhitaji na mpeleke huduma”amesema Majaliwa.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 30, 2022
Selasini aomba Mahakama imuongeze muda