Rais wa Gambia, Adama Barrow ametangaza kifo cha Makamu wake, Badara Alieu Joof (65), ambaye amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya muda mfupi akiwa nchini India.

Joof, aliteuliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi 2022 na aliwahi kuhudumu kama waziri wa elimu kutoka 2017 hadi 2022.

Makamu wa Rais wa Gambia, Badara Joof wakati alipokuwa akitoa hotuba katika mkutano wa viongozi wa hali ya hewa COP27 nchini Misri Novemba 7, 2022. Picha ya Ahmad Gharabali/AFP

Makamu huyo wa rais, alikuwa ameondoka Gambia takriban wiki tatu zilizopita kwa matibabu, na hakuwa ameonekana hadharani kwa miezi kadhaa kabla ya safari hiyo.

Joof, alikuwa naibu wa nne kuhudumu chini ya Barrow tangu ushindi wake wa kihistoria mwaka wa 2016 dhidi ya mwanajeshi wa zamani Yahya Jammeh na kuapishwa mwaka uliofuata, na wa pili tangu rais ashinde tena uchaguzi mwaka 2021.

Mbeya City wapinga kadi nyekundu, penati
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 19, 2023