Rais wa Guinea ya Ikweta, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ametawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 43, anatarajia kuwania muhula mpya wa uongozi katika uchaguzi wa urais wa Novemba 20, 2022.

Makamu wa rais wa nchi hiyo, ambaye pia ni mtoto wa Rais, Teodoro Nguema Obiang Mangue ameuarifu umma kupitia chapisho la kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema, baba yake mwenye umri wa miaka 80, atawania tena muhula unaofuata.

“Kwa sababu ya haiba yake, uongozi wake na uzoefu wake wa kisiasa”, chama tawala kwa kauli moja kilimchagua Obiang kama mgombeaji wake katika uchaguzi wa Novemba 20.” ameandika Nguema Obiang Mangue kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Guinea ya Ikweta, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo (80), Picha na newzimbabwe.com

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo (80), ndiye mkuu wa nchi anayekimbizana na Rais wa Cameroon Paul biya kwa kungoza nchi kwa muda mrefu zaidi duniani ukiondoa utawala wa kifalme ambapo yeye anafikisha miaka 43 ya utawala na Biya anafikisha miaka 47 ya utawala ukichanganya na miaka yake saba ya uwaziri mkuu.

Obiang, na Chama chake cha Democratic Party of Equatorial Guinea (PDGE) kinashikilia viti 99 kati ya 100 katika bunge la chini hiyo linalohodhi viti vyote 70 vya seneti, na bado haijawekwa wazi nani mwingine anatarajia kuwa mgombea wa chama hicho katika kura ya urais.

Vyombo vya Habari vya nchi hiyo viliwahi kuripoti kuwa, mtoto huyo tajiri ambaye ni makamu wa rais Nguema Obiang Mangue aliyepewa jina la utani “Teodorin”, aliandaiwa kugombea katika uchaguzi huo lakini hata hivyo, hakuchaguliwa kugombea nafasi hiyo.

Ebola Uganda: Kesi zaongezeka, vifo vyafikia 11
Nini kitatokea ikiwa Putin atatumia silaha za Nyuklia?