Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda  leo Novemba 6, 2016 amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya vituo vya Polisi  na kujionea hali halisi ya vituo hivyo ambavyo vimekuwa vikifungwa mapema  kwa sababu yua upungufu wa askari katika vituo hivyo.

Makonda amesema kuna uhaba mkubwa wa polisi kulingana na watu ambao wanawahudumia na kuongeza kuwa uhalifiu umeongezeka na kusema kuna haja ya kuongeza nguvu  katika suala zima la usalama wa raia na mali zao.

Aidha, ameongeza kuwa ana mpango wa kujenga  vituo vya polisi  ishiririni katika jiji la Dar es salaam ambavyo vitaweza kuwa na askali mia moja  kila kituo kimoja  ambao wataweza kuhudumia watu laki Nne kwa siku, na kusema kuwa mpango huo wa kujenga vituo hivyo utasaidia kuongeza muda wa kutoa huduma kwa wananchi na kuongeza uhakika wa usalama kwa wafanya biashara kufanya biashara zao kwa uhuru  zaidi.

Kituo kimoja kitakuwa na uwezo wa  kuhudumia wananchi kulingana na idadi ya watu wa eneo husika ambapo  kila kituo kitagharimu kiasi cha shil. mil 500 na vituo vyote vinatarajiwa kugharimu kiasi shil. bil. moja.

FBI: Clinton hana kosa la kujibu
Jokate aichambua show ya Ali Kiba Fiesta, “Hushindani na yeyote TZ”