Wanahabari wametakiwa kutoiogopa na kukatishwa tamaa na vifungu vichache vya Sheria  ya Habari iliyosainiwa na Rais John Magufuli hivi karibuni na badala yake wanatakiwa kuisoma na kuieleawa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga wakati wa mkutano wa siku mbili uliowakutanisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Mkutano huo wa wahariri umelenga kupitia sheria ya vyombo vya habari na kujadili mpango mkakati wa TEF, wa kuendeleza tasnia ya habari huku wakipata uzoefu kutoka nchi za Kenya na Afrika ya kusini.

“Kama tuliweza kuishi na sheria ya magazeti ya mwaka 1976 basi tunaweza hata chini ya hii sheria mpya,kwa sababu hii sheria ni afadhali kuliko ile ya mwaka 1976, imepunguza vitu vingi sana ambavyo alikuwa amepewa mtu mmoja na badala yake kuhamishiwa kwa bodi”alisema Makunga.

Aidha, Makunga amesema kuwa katika muswaada wa habari suala la elimu lilionyesha ni lazima mwandishi afike ngazi ya stashahada huku sheria ikiwa haijaonyesha kipengele hicho.

Hata hivyo amesema tayari sheria imesha sainiwa kinachotakiwa ni kuona namna ya kuendesha tasnia ya habari na kuimarika chini ya sheria hiyo bila kuathiri uendeshaji wa taaluma ya habari.

Abiria wailalamikia Udart
JPM afanya uteuzi na mabadiliko katika wizara na mikoa