Wakati wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika, Young Africans wakijiandaa kucheza na APR ya Rwanda mwishoni mwa juma lililopita kule jijini Kigali, mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Simba Haji Manara alitupa bomu katika mitandao ya kijamii baada ya kukerwa na tambo na watani zao wa jadi kwa kujiita WAKIMATAIFA.

Manara alirusha bomu hilo, kwa kuamini watani zao wa jadi hawana hadhi ya kujiita hivyo kutokana na historia kubwa ambayo iliwahi kuwekwa na klabu ya Simba miaka kadhaa iliyopita.

Ifuatayo ni taarifa (Bomu) iliyotolewa na Haji Manara ambayo aliilenga kwa makusudi iende upande wa pili wa shilingi.

 

KUTOKA KWA HAJI MANARA

Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi.kuna neno wa kimataifa hulisikia likiimbwa..

Waimbaji wakuu wa neno hilo ni washabiki wa yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.

Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa mchangani au wamatopeni.wengi wananilaumu kuwa kwa nn huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa yanga.jibu langu ni jepesi tu.lazma tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.

Mm hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni.haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki maandazi.

Kwa hyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni.always nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo.

Na wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halaf zifananisheni na timu nyingine nchini

Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya.

Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii ktk kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.

 

  1. Simba ndio timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa.ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
  2. Simba ndio timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam
  3. Simba ndio timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini navy ya afrika kusini.
  4. Simba ndio timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyew na hili lilinuliwa mwaka1968.
  5. Simba ndio timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyew na hili lilizinduliwa 1971.
  6. Simba ndio timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966
  7. Simba ndio timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.
  8. Simba klabu ya kwanza nchini kwenda ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.
  9. Simba ndio timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.
  10. Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa afrika mashariki na kati.ndio timu iliochukua ubingwa mara nyingi kupita klabu yoyote afrika mashariki na kati nzima(champs off all time)
  11. Simba ndio timu pekee nchini iliowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa afrika na hii ilikuwa1974.
  12. Simba ndio timu pekee nchini na afrika mashariki kufika fainali ya kombe la caf na hii ilikuwa1993.

13.Simba ndio timu inayoshikilia rekodi afrika kama si duniani kwa kufungwa na mufurila wonderes ya Zambia goli nne kwa bila na kwenda kuibamiza tano bila kwao.mbele ya rais wao Kenneth Kaunda.hii haijafanywa na klabu yoyote afrika na nna mashaka duniani.hii ilikuwa 1979.

  1. Simba ilicheza ktk hatua ya makundi ya klabu bingwa afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.
  2. Simba ndio timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwa afrika nadi zamalek hii ilikuwa pia 2003.
  3. Simba ndio klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu.kuanzia
  4. waliowatoa mwaka jana etoile du sahel.Tunisia
  5. Widad Casablanca ya Morocco
  6. El setif Algeria
  7. El harach Algeria
  8. Halafu tumezifunga timu zote kubwa za misri.zamalek.al ahly.Arab contractors. Ismailia.mehala al kubra na timu nyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.
  9. Pia imeshaitoa el merekh ya Sudan 1994 ktk klabu bingwa ya afrika.
  10. Simba pia imeshazifunga miamba ya afrika ya afrika magharibi.kuanzia asec.asante kotoko.hafia ya guinea.na hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia nkana red devils.
  11. Tukirudi juu Simba ndio timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.
  12. Simba ndio klabu pekee nchini kujenga jengo lake lenyew kwa nguvu za wanachama na washabiki.wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee karume100%,Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya sabini.
  13. Angalia idadi ya wachezaji wa Simba walioenda ulaya kucheza soka la kulipwa.

Nico njohole, Deo njohole, Kassim matitu na George Kulagwa

Huku ikiwa na makumi ya nyota wake kadhaa waliowah kutapakaa sehem mbali mbali duniani.

Nikutajie wachache.

Khalid Abeid, Haidar Abeid, Martin Kikwa, Athman Mambosasa, Zamoyoni Mogella, Hamis Gaga, Lilla Shomari, Iddi Pazi, Kiwelu Mussa, George Masatu Hussein Masha na wengine wengi, bila kumsahau nguli wa sasa Mbwana Samata (Mutoto Ya Msimbazi).

Na hapa kumbukumbu ikae vizuri wazee wangu mimi Sunday na Kassim Manara wakati wanaenda kucheza Ulaya hawakuwa wachezaji wa Yanga, walikuwa wakicheza Pan African.

  1. Nimalizie kwa kuwaambia FIFA ilizitaja timu bora za karne kwa kila nchi.kwa Tanzania Simba ilitajwa ndio timu bora ya karne na wenye mpira wao FIFA.

Nenda kwenye rekodi za CAF ndio utajua nani wa kimataifa baina ya cc na wao.

Porojo za mjini ntakuwa nimezimaliza sasa.na anayebisha abishe kwa data.

Wakoloni wetu walitufundisha hv…

No reaserch no data no right to speak.tafsiri isio rasmi.hujafanya utafiti na huna takwimu funga bakuli lako.

Asanteni na nendeni mkawaambie.

Haji S Manara

Msemaji wa klabu bora ya muda wote Tanzania (best club of all time)

Ukiona errors zipotezee jadili issues na nnaruhusu challenges kama zipo

Porojo peleka kuleeeeeee.

Baada Ya Ushindi Wa Tatu Bila, Stewart Hall Aahidi Mazito
Dk. Kigwangalla awapa pole Chadema uteuzi wa Katibu Mkuu, adai wao walimtenga