Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amemchambua Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vicent Mashinji ambaye alisoma nae Chuo Kikuu.

Dk. Kigwangalla amekanusha sifa mbalimbali ambazo Katibu Mkuu huyo mpya amekuwa akitajwa kuwa nazo tangu alipotangazwa wikendi hii.

Moja kati ya sifa alizozikana ni pamoja na kuwa na msimamo akieleza kuwa mwaka 2005 alishindwa kuhimili vishindo Chuoni na kwamba Kamati Kuu ya mgomo ambayo Kigwangalla pia alikuwa mjumbe iliamua kumtenga.

Kada huyo wa CCM amewapa pole Chadema kama walitumia sifa hizo kumteua Dk. Mashinji kuchukua nafasi iliyoachwa na Dk. Wilbroad Slaa. Mashiji alipishwa na asilimia 100 ya wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema baada ya kuangazwa. Anadaiwa kuwa ndiye alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Wanataaluma ya Ukawa katika uchaguzi Mkuu uliopita.

Hivi ndivyo Dk. Kigwangalla alivyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mapema leo:

“Ndg., Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa mimi na Dkt. Ulimboka, na hakuwahi kuongoza mgomo, sema alishiriki mgomo ulioongozwa na mimi na Dkt. Ulimboka. Kiukweli, ni mwanasiasa mzuri, msemaji, msomi mzuri (tumesoma naye MBA chuo kimoja), sina hakika kama alimaliza masomo ya Ubingwa maana alinyanyaswa na Supervisor wake, akasusa akaamua kujiiunga masomo ya MBA, na sina hakika sana kuhusu ‘msimamo usiotetereka’. Maana baada ya vitisho vya 2005, aliyumba sana na tulimtenga na ku-aVoiD kumualika vikao vya CC ya mgomo. Hivyo, kama kiGeZo kilikuwa ni hii Historia, pole kwa CHADEMA.”

Manara Akerwa Na Yanga Kujiita Wakimataifa
Mbeya City Kujiuliza Kwa Africans Sports Leo