Wiki hii moja ya habari kubwa katika mitandao inayoripoti habari za michezo nchini na barani Africa ni aliyekuwa msemaji wa Simba SC Tanzania Haji Manara kujiunga na Yanga,

Hii habari imepokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wengi na wadau mbalimbali wa soka barani Afarika wekiwemo watangazaji na wachambuzi wa soka barani Africa

Kwa upande wa Mtangazaji mashuhuri wa soka nchini Misri @Muhammad El shazly, yeye amewataka mashabiki wa Simba kutokuwa na hofu yeyote kwani wachezaji, makocha na wasemaji au watungine wanakuja na kuondoka katika klabu lakini mashabiki wao daima wataendelea kubaki na klabu yao.

“Kwenu mashabiki wa Simba, mashabiki pekee ndio watabaki kusimama na klabu yao, wachezaji, makocha na wasemaji wanakuja na kuondoka lakini mashabiki watabaki kuwa mtaji wa klabu kwasababu ya mapenzi yasiyopimika kwa klabu yao alisema Muhamma El Shazly

Waziri Mkenda atoa maagizo bodi ya korosho
Simba SC yamuaga rasmi Luis Miquissone