Mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Manuel Agudo Durán Nolito amekua mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu ya Manchester City chini ya utawala wa meneja mpya Pep Guardiola.

Manchester City iliatangulia kumsajili kiungo kutoka nchini Ujerumani ambaye alikua akiitumikia klabu ya Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan.

Nolito amejiunga na Man city akitokea nchini kwao Hispania alipokua akiitumikia klabu ya Real Club Celta de Vigo, ambayo msimu uliopita aliisaidia kuifungia mabao kadhaa na kuwezesha kumaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

“Nitajaribu kufanya kila linalowezekana ili kusaidiana na wenzangu na kufanikisha mafanikio ya klabu hii,”

“Najua kutakua na changamoto mpya katika maisha yangu ya soka nchini England, ila sinabudi kufanya jitihada ili nikabiliane nazo na tuweze kufanikisha maazimio ya Man city, Amesema Nolito alipozungumza na mwandishi wa tovuti ya Man City.

Nolito alianza kuitumikia Real Club Celta de Vigo mwaka 2013 akisajiliwa kutoka nchini Ureno alipokua akiitumikia klabu ya Benfica, na kwa kipindi chote alichokuwepo Balaídos amefanikiwa kucheza michezo 100 na kufunga mabao 39.

Chelsea Yawatema Rasmi Falcao, Pato Na Amelia
Themi Felix Asajiliwa Tena Kagera Sugar