Halmashauli ya Manispaa ya Ilala wamemuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya usafi katika soko la feri lililopo jijini Dar es salaam ukiwa ni muendelezo wa agizo la  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wa kutaka kubuni kitu cha kufanya siku ya maadhimisho.

Hayo yamesmwa na Katibu tawala wa Manispaa hiyo Edward  Mpogolo alipokuwa akizungumza na dar24.com, amesema kuwa wameamua kufanya usafi ili kumuenzi baba wa taifa sababu mwalimu alipiga vita suala zima la maradhi, hivyo kufanya kwao usafi ni kuenzi kile ambacho baba wa taifa alikipinga.

Aidha Mpogolo ameongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu  ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria  za Manispaa hiyo zinazo husu masuala ya mazingira na kuagiza watendaji wote kusimamia usafi katika manispaa hiyo kwani ndiyo kitovu kikuu cha biashara nchini na serikali kwa ujmla.

Tumeamua kubuni kitu cha kufanya ili kumuenzi Baba wa Taifa kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, si hivyo tu bali Baba wa Taifa pia alipiga vita sana maradhi hivyo kufanya kwetu usafi tunaenzi kile Mwalimu alikipinga kwa nguvu zote na ukizingatia hili ni soko ambalo linahudumia watu wengi sana” Alisema Mpogolo.

TBS waangushiwa 'tofali’ kashfa ya kuvushwa kontena 100 bandarini
Majaliwa apokea msaada wa sh. mil. 27.62, Tetemeko Kagera