Mlinda mlango wa FC Bayern Munich, Manuel Neuer ameliomba benchi la ufundi la Man Utd kufikiria upya suala la kumtumia kiungo Bastian Schweinsteiger ili kusaidia kupunguza makali ya upinzani unawakabili katika ligi ya Engalnd.

Neuer amewasilisha ombi hilo kwa njia ya vyombo vya habari huku ikifahamika dhahir Jose Mourinho hana mpango wa kumtumia Schweinsteiger kwa kigezo cha kutokua sehemu ya mikakati yake tangu alipotua Old Trafford miezi minne iliyopita.

Neuer, amesema ipo haja kwa suala la mchezaji huyo kutiliwa maanani kutokana uwezo wake kisoka kufahamika vizuri duniani kote, na anaamini ataweza kusaidia kupunguza makali ya upinzani uliopo.

Hata hivyo mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 30, anaamini ombi lake litasikilizwa na benchi la ufundi la Man Utd na kufanyiwa kazi.

“Ninamatarajia kuona jambo hili linapokelewa na kufanyiwa kazi, kwa sababu ninaamini Bastian ni sehemu ya kikosi cha Man Utd na anaweza kufanya jambo fulani atakapopewa nafasi.

“Sote tunafahamu uwezo wake bado upo juu na kwangu ninaamini Bastian ni mmoja wa viungo wenye ubora duniani”. Alisema mlinda mlango huyo.

Video: Onyesho la magari Tanzania 'Autofest' kufanyika Oktoba 28
Mabadiliko Ya Simba SC, Yanga SC Yapigwa Stop