Rais Donald Trump, amesaini amri ya kuifanyia mageuzi idara ya polisi nchini Marekani wakati nchi hiyo ikiwa inagubikwa na maandamano, kufuatia mauaji ya wamarekani weusi mikononi mwa maafisa wa polisi.

Trump amesema wanapaswa kuachana na mbinu za zamani ambazo zimefeli, na kwamba kinachohitajika sasa si hofu na migawanyiko, bali kuimarisha uzingatiaji wa sheria na kuzileta jamii pamoja.

Amri hiyo ya Rais inatoa ufadhili kwa idara ya polisi kote nchini humo, na inapiga marufuku mbinu ya polisi kumkabili mshukiwa kwa njia inayomfanya asiweze kupumua kama hatua ya kumdhibiti, ila tu ikiwa maisha ya polisi yako hatarini.

Hata hivyo amri hiyo pia inahimiza mafunzo zaidi kuhusu miongozo ya kutumia nguvu, na pia ukusanyaji wa taarifa au data za polisi ambao wamejihusisha na mienendo mibaya.

Young Afrcans wabanwa Dodoma
Takukuru yatoa onyo kwa wagombea watoa rushwa