Mshambuliaji kutoka nchini Italia na klabu ya Nice ya Ufaransa, Mario Balotelli ameelezea ugumu aliokutana nao mbele ya meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Balotelli ametoa kauli ya kutomfahamu kabisa Klopp, kuonesha kutokuwa na uhusiano na meneja huyo kutoka nchini Ujerumani.

Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za AC Milan, Inter Milan na Manchester City ameelezea asingeweza kupata nafasi chini ya Klopp kwa kuwa hawakuwa na uhusiano wowote.

Amenukuliwa akisema: ” Klopp? Simfahamu. Aliniambia niondoke kwa mkopo Liverpool na kurejea baadaye. Nikamwambia asante na kwaheri.”

Balotelli ameanza vizuri maisha mapya katika klabu ya Nice kwa kufunga mabao 5 ndani ya michezo sita.

Young Africans Wabisha Hodi Kisiwani Unguja
Tyson Fury Amkacha Rasmi Wladmir Klitschko