Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa kike nchini kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao, ambapo amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa Wilayani Mbozi, ambapo amewaasa kuwa masomo ni ufunguo wa maisha ambao utawasaidia katika maisha yao.

“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara kwa ajili ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu, kuweni makini sana kwa sababu umri wenu bado ni mdogo sana,”amesema Marry.

Amesema kuwa ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke, hivyo amewataka kuzingatia masomo na maadili.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wanafunzi hao kama wakizingatia masomo na kusoma hadi elimu ya Juu watakuwa na uwezo mkubwa wa kutambua lipi ni jambo jema na lipi ni jambo baya.

Wanasheria na wakaguzi wa mazingira wapigwa msasa
Gambo awanyooshea kidole wanaoingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo