Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini England (FA) Martin Glenn ametangaza msimamo wa chama hicho kuhusu pendekezo la kusimamisha michezo ya ligi wakati wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Glenn amesema pendekezo hilo halikubaliki na wameona bado kuna umuhimu wa michezo ya ligi ambayo imepangwa katika tarehe za sikukuu za mwishoni mwa mwaka iendelee kama ilivyopangwa.

Amesema wamekua na majadiliano ya kina na mameneja wa klabu za ligi kuu, na wamekubaliana wazi suala hilo liwekwe pembeni.

Hata hivyo Glenn amethibitisha kuwepo kwa mapendekezo mengine ya kusimama kwa michezo ya ligi ya England itakapofika mwezi Januari katika kila msimu, ambayo bado yanafanyiwa mpango wa kujadiliwa.

Ligi ya England imekua inaendeshwa tofauti na ligi zingine barani Ulaya ambazo kwa asilimia kubwa michezo yake husimama kupisha sikukuu za mwishoni mwa mwaka, ili kutoa nafasi wachezaji kupumzika sambamba na kujiunga na familia zao kwa ajili ya kusheherekea.

Wenger Awavuruga FC Barcelona, Waanza Kumfikiria Glen Johnson
Kigogo wa polisi, afisa wake watumbuliwa kwa kukutwa na magari ya wizi