Mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona weameonyesha dhamira ya kutaka kumsajili beki wa pembeni wa klabu ya Stoke City ya nchini England, Glen Johnson.

Johnson, mwenye umri wa miaka 32, ameonekana huenda akawa suluhisho la tatizo la beki wa kulia katika klabu hiyo ya Hispania, ambayo miezi minne iliyopita ilimpoteza Dani Alves aliyetimkia Juventus FC.

Mipango ya usajili wa beki huyo ambaye aliwahi kucheza katika klabu za Chelsea na Liverpool, huenda ikafanyika mwezi januari 2017 wakati wa dirisha dogo la usajili.

Hata hivyo bado kuna mvutano wa kufanyika kwa maamuzi ya mwisho ya usajili wa mchezaji anaecheza nafasi beki wa kulia, kutokana na orodha ya wachezaji ambayo ipo mezani kwa meneja wa FC Barcelona, Luis Enrique.

Majina ya wachezaji yaliyowekwa mezani kwa meneja huyo ni Darijo Srna (Shakhtar Donetsk), Stephan Lichtsteiner (Juventus), Pablo Zabaleta (Manchester City) pamoja na Branislav Ivanovic (Chelsea).

Pamoja na uwepo wa changamoto hiyo, bado jina la Johnson limeonekana kuchukua nafasi kubwa.

Mipango hiyo ya FC Barcelona inadhihirisha wamekata tamaa ya kumrejesha nyumbani beki wa pembeni wa Arsenal Héctor Bellerín Moruno.

FC Barcelona walionyesha dhamira ya kweli ya kutaka kumsajili beki huyo aliyeondoka Camp Nou mwaka 2011, lakini msimamo mkali uliotangazwa na meneja wa Arsenal Arsene Wenger majuma mawili yaliyopita, wa kutokuwa tayari kumuachia Bellerín umevuruga mipango yao.

Roberto Mancini Akunwa Na Kiwango Cha Balotelli
Martin Glenn: Michezo Ya PL Itaendelea Mwishoni Mwa Mwaka