Mashabiki 45 wa klabu ya Simba usiku wa kuamkia leo walianza safari ya kuelekea mjini Lusaka Zambia, kwa ajili ya kuishangilia timu yao katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows.

Simba SC ilishinda mchezo wa Mkondo wa kwanza uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam Jumapili (Novemba 28), kwa mabao 3-0.

Msaidizi wa Afisa Habari wa Simba SC Ally Sharty amezungumza na Dar24 Media na kuthibitisha safari ya Mashabiki hao kuelekea mjini Lusaka.

Sharty amesema mbali na Mashabiki, Msafara huo umewajumuisha baadhi ya Waandishi wa Habari wanaokwenda kuripoti mchezo wao wa Jumapili (Desemba 05).

“Msafara wa Mashabiki na baadhi ya Waandishi wa Habari ulianza jana usiku kwa basi la klabu ya Simba SC, unatatarajia kuwasili mjini Lusaka leo jioni.” amesema Sharty.

Katika mchezo wa Jumapili (Desemba 05), kikosi cha Simba SC kitalazimika kusaka ushindi ama matokeo ya sare ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya Makundi, huku wenyeji wao Red Arrows wakihitaji ushindi wa mabao 4-0 na kuendelea.

Simba SC kuzikwepa changamoto Lusaka
Mtibwa Sugar kurudi Manungu Stadium