Afisa Habari wa Timu ya Mashujaa inayoshiriki Championship, Benson Mwangatwa amefunguka kuwa timu yao ina imani kubwa kuelekea mechi yao ya mkondo wa pili hatua ya mtoano dhidi ya Pamba unaotarajiwa kupigwa mwishoni mwa juma hili katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma mwishoni mwa juma lililopita, Mashujaa ilipata ushindi wa mabao 4-0, huku mshindi wa jumla akitarajiwa kucheza playoff na timu ya ligi kuu.

Mwangatwa amefunguka: “Kikosi kinaendelea na maandalizi ya mwisho kabla hatujaanza taratibu za kuelekea Mwanza, hali ya wachezaji, benchi la ufundi ipo vizuri kabisa, morali ipo juu na tunaimani kubwa ya kupata ushindi endapo tukipambana.

Wenye Saratani waomba kuondolewa ushuru
Kocha Kitayosce afunguka usajili 2023/24