Meneja kutoka Argentina Mauricio Pochettino amekamilisha mpango wa kujiungana mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG), kwa kusaini mkataba ambao muda wake unaendelea kuwa siri.

Fabrizio Romano mwandishi mkongwe kutoka Italia amefichua siri ya meneja huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs kujiunga na mabingwa hao wa Ligue 1, kwa kusema pande hizo mbili zilifikia makubaliano na kusaini mkataba jana Jumapili Desemba 27.

PSG wamefikia maamuzi ya kumuajiri Pochettino, baada ya kutangaza kumtimua  Thomas Tuchel mwishoni mwa juma lililopita, kufuatia mwendo mbovu wa timu hiyo. 

Tuchel alifutwa kazi muda mchache akitoka kuongoza kikosi chake kushinda mabao 4-0 dhidi ya  Racing Strasbourg.

Pochettino amekuwa nje kwa muda mrefu bila kuwa na timu baada ya kutimuliwa  na uongozi wa Totenham Hotspursmwaka 2019 , na amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na FC Barcelona, Manchester United na Real Madrid.

Majengo chakavu Zanzibar kufungwa
Chama abembelezwa kusaini mkataba mpya Simba SC