Klabu ya Tottenham Hotspur haitopinga mashtaka yanayomkabili kiungo Moussa Sissoko ambaye amewekwa kikaangoni na chama cha soka nchini England FA, kufuatia sakata la kumpiga kiungo wa Bournemouth Harry Nicholas Arter.

Meneja wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino, amesema uongozi umejiridhisha kwa kuangalia picha za televisheni za mchezo wao dhidi ya Bournemouth na kuna jambo ambalo wamelibaini lilifanyika baina ya Moussa Sissoko na Harry Nicholas Arter.

Sissoko, ambaye aliingia uwanjani kama mchezaji wa akiba alionekana akimpiga kwa kiwiko Arter, lakini mwamuzi hakuona tukio hilo.

Tayari FA wameshamfungulia mashataka kiungo huyo kutoka nchini Ufaransa, na wamemtaka kuwasilisha utetezi wake kabla maamuzi dhidi yake hayajachukuliwa.

Image result for Moussa Sissoko and Harry Nicholas Arter on sky sportsHarry Nicholas Arter (Alielala chini) Akiugulia maumivu baada ya kupigwa kiwiko na Sissoko (Alieshika mpira).

“Tumeona kupitia picha za televisheni, na tumebaini Sissoko alifanya tukio lile kwa makusudi kutokana na kiwiko cha mkono wake kuelekea usoni mwa Arter.

“Ni kweli kiwiko kilitumika na hilo hatutolipinga kamwe, tumekubaliana na hali halisi, na sasa tunasubiri hukumu itakayotolewa na FA.” Alisema Pochettino alipozungumza na waandishi wa habari.

Endapo Sissoko atakutwa na hatia, huenda akafungiwa michezo mitatu iliyo chini ya chama cha soka nchini England (FA) na adhabu hiyo itaanza katika mchezo wa leo wa kombe la ligi ambapo Spurs watapambana na Liverpool, na kisha mchezo wa mwishoni mwa juma dhidi ya Leicester City pamoja na Arsenal ambao utachezwa mwishoni mwa juma lijalo.

Wakati huo huo Pochettino amethibitisha atamuanzisha mlinda mlango Michel Vorm katika mpambano wa leo dhidi ya kikosi cha Juergen Klopp, huku Toby Alderweireld akitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Spurs kufuatia kupona majeraha.

Tofauti ya idadi ya wapiga kura yamtesa Bulaya Mahakamani
Babu Hans van der Pluijm Anukia Azam Complex