Mawaziri 15 wa Nchi  Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC), wanatarajia kufanya mazungumzo kesho jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa mawaziri hao wanatarajiwa kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo elimu, ushiriki wa nchi za SADC, ikiwa ni pamoja na kuzungumzia hali inayoendelea nchini Msumbiji.

“Tanzania ni  mwenyeji na mwenyekiti wa Mkutano huo, ambapo pia inaongoza Kitengo Maalumu cha Masuala ya Ulinzi,Usalama pamoja na Siasa, pia kamati ya siasa na diplomasia inatarajiwa kukutana  wiki hii” amesema Waziri Mahiga.

Kila mwaka mawaziri hao hukutana mara moja, kwa lengo la kuzungumzia masuala  mbalimbali yanayohusu nchi wanachama wa umoja huo.

Katika hatua nyingine,  Waziri Mahiga amesema kuwa ,Tanzania  inashirikiana na  Msumbiji kufanyia kazi suala la  watanzania waliohamishwa nchini humo.

“ Hili ni suala gumu kidogo tusitoe majibu rahisi, na hivyo Serikali zote mbili zinaendelea kufanya mazungumzo zaidi juu ya suala hili” amesema Waziri Mahiga

Nasser Al Khelaifi: Marco Verratti Hauzwi
Video: Rais wa Uganda, Shelisheli kutembelea Tanzania