Kocha wa vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Wekundu Wa Msimbazi Simba, Jackson Mayanja amesita kuzungumzia suala la ubingwa licha ya kikosi chake kuonyesha dhamira ya kuuwania kwa msimu huu.

Mayanja amesita kulizungumza suala hilo, baada ya kuulizwa kama ana uhakika wa kuirejesha heshima ya ubingwa Msimbazi, ambayo imepotea kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Kocha huyo kutoka nchini Uganda, amesema ni mapema mno kuzungumza suala la ubingwa ambao pia unapigiwa upatu na klabu nyingine mbili za Young Africans pamoja na Azam FC.

“Ukiuzungumzia ubingwa kwa sasa utakuwa unajidanganya kwa sababu hao tuanofukuzana nao pia wapo katika hali nzuri, kwa hiyo yeyote anaweza kuuchukua”.

“Ukiangalia hali ilivyo utaona kabisa kwamba Yanga na Azam kwa alama walizonazo pia wanaweza kumaliza katika nafasi ya kwanza, hivyo ukinitaka mimi niseme kama Simba itakuwa bingwa au la, nitashindwa kukuhakikishia hilo, Alisema kocha Mayanja.

Mayanja amekua akipewa matarajio makubwa ya kufikia lengo la kutwaa ubingwa akiwa na klabu ya Simba, baada ya kuonyesha mabadiliko ya kiushindani tangu alipokabidhiwa kikosini mwanzoni mwa mwaka huu, kufuatia kuondoka kwa kocha kutoka nchini England Dylan Kerr.

Mashabiki Wa Aston Villa Watimiza Lengo Kwa Remi Garde
Newcastle Utd Wapata Pigo Juu Ya Pigo