Mtendaji mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba, Senzo Masingiza amewataka mashabiki na wanachama kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki, ambacho kimegubikwa na tetesi nyingi za usajili.

Simba SC inahusishwa kuwa kwenye mawindo ya kuwasajili wachezaji kadhaa wa kimataifa, kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao kwa msimu ujao wa ligi ya Tanzania bara na michuano ya kimataifa.

Mazingiza amesema anatambua mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wanatamani kuona timu yao ikifanya maboresho ya kikosi kwa kusajili wachezaji wenye viwango vikubwa, ambao wataleta ushindani dhidi ya timu nyingine za Tanzania na kimataifa.

Kiongozi huyo kutoka Afrika kusini amesema lengo kubwa la Simba SC ni kuwa na timu bora, huku akisisitiza uongozi wa klabu hiyo kwa sasa unaendelea na shughuli mbalimbali za kimaendeleo, sambamba na kushirikiana kwa ukaribu na benchi la ufundi, hivyo mashabiki na wanachama wanatakiwa kuwa watulivu.

“Mashabiki siku zote wanataka kuona timu ikisajili kila baada ya dirisha kufunguliwa wakiamini timu bila kusajili haitafanya vizuri, sitaki kusema kuwa hatutasajili ila mipango yote ya kuhakikisha timu inakuwa bora ipo kwa viongozi ambao tunashirikiana kwa ukaribu na benchi la ufundi.”

 “Hakuna kiongozi wala benchi la ufundi la timu ambalo lipo tayari kuona timu haifanyi vizuri, hivyo malengo ambayo siku zote kila Mwanasimba huyatamani kuyapata haswa yale ya kimataifa ambayo bado hayatimia,” –

Wachezaji wa kigeni ambao wanatajwa kuwaniwa na Simba SC ni:

1. Mghana – Yakubu Mohammed ( beki wa kati ) – Azam Fc, Tanzania.

2. Mburkinabe – Yacouba Sogne ( mshambuliaji ) – Asante Kotoko, Ghana.

3. Mzambia – Justine Shonga ( winga ) – Orlando Pirates, Afrika Kusini.

4. Mkenya – Mike Kibwage _ MK12 ( Beki wa kati ) – KCB ( Captain ), Kenya.

TFF yafafanua Dola za FIFA
Hija Ugando: Nilishindwa kucheza Tunisia, Italia