Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linawashikilia Nassor Issa Nassor miaka (30), Omar Hamad Nassor miaka (27) na Mzee wa miaka (65) kwa tuhuma za kunajisi watoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Saidi amesema “ili watuhumiwa waweze kutiwa hatiani kunahitajika ushirikiano kutoka kwa wananchi kwa kutoa ushahidi kwenye vyombo vya sheria wanapohitajika”

Aidha amebainisha kuwa Mzee wa miaka (65) mkazi wa Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete anadaiwa kutenda kosa hilo julai 28, 2020 kwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (14), Nassor Issa Nassor mkazi wa Kizimbani Wete anadaiwa kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka (8) Julai 26, 2020 na Omar Hamad Nassor mkazi wa Bwagamoyo Mtambwe anadiwa kumuingilia mtoto wake wa kambo.

Hata hivyo Kamanda Saidi amesema watuhumiwa wote bado wanashikiliwa na Jeshi Polisi wakisubiri upelelezi ukamilike na kufikishwa Mahakamani.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete , Haroub Suleiman ameiomba jamii kuwa na malezi ya pamoja ili kila mzazi amuone mtoto wa mwenzake kuwa ni wake.

Wanafunzi wanusurika kifo Bweni likiteketea kwa moto
Makamu wa Rais Kufungua maonesho ya Nanenane