Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amemtaka Rais John Pombe Magufuli aende mkoani Kagera, Kuwafariji watanzania waliothirika na tetemeko la ardhi.

Mwenyekiti huyo alishangazwa na Rais Magufuli kushindwa kufika Bukoba kuwafariji waliokumbwa na tatizo hilo hadi sasa ilihali alihairisha safari ya kwenda nchini Zambia kuhudhuria kikao cha Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kwa ajili ya  kuwahudumia walioathirika na janga hilo.

Alisema, rais anatakiwa kufahamu kuwa matukio kama hayo yaliotokea Bukoba mkuu yeyote wa nchi anayefahamu anatakiwa kwenda kuwafariji wananchi wake na kutoa misaada ya hali na mali.

Mh.Mbowe alisema hadi sasa  hakuna hata msaada mmoja uliotolewa na serikali zaidi ya kupiga harambee kukusanya fedha na misaada kutoka kwa watu mbalimbali. Hivyo aliisihi serikali kujiandaa kuwa tayari kwa lolote kwa maana majanga hayana muda wala taarifa ni muda wowote yanaweza kutokea .

Yemi Alade amtamani Ali Kiba
Vyama 12 vyataka JMP kuondoa zuio, vyatishia kutoa tamko zito