Mchungaji mkuu wa kanisa la Church of God Kabindi Mchungaji Daudi Bonze pamoja na waumini wa kanisa hilo wamemshukuru na kumpongeza Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi kwa kutiiza ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa kanisa ikiwa ni kuunga mkono jitihada za waumini hao.

Mchungaji Daudi ameyanena hayo mara baada ya kupokea mifuko 50 ya Saruji ikiwa ni ahadi aliyoitoa Mhandisi Ezra Chiwelesa na kusema kuwa wamepokea kwa mshangao mchango huo kwa kuwa walikuwa wakipigwa danadana na viongozi wa kisiasa kama yeye waliomtangulia na kuongeza kuwa hawakuamini kama hili litatekelezwa kwa uharaka namna hii.

Daudi ameongeza kuwa maneno ya mungu yanasema kuwa: “Atawalapo mwenye haki Taifa huinuliwa sana, na leo maneno hayo tunayashuhudia hapa na kwingineko kote, mbunge huyu amekuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi na kwa jamii anayoiongoza, sisi kama viongozi wa dini jukumu letu ni kumuombea kwa Mungu aweze kumuongoza kwenye njia iliyonyooka.”

Julai 25, mwaka huu, Mbunge wa jimbo la Biharamuo Magharibi Mhandisi Ezra John Chiwelesa alisali katika kanisa hilo na kushuhudia harambee kubwa ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya, ambapo alitoa shilingi laki tano fedha taslimu na kuahidi kuleta mifuko hamsini ya Saruji na kuutaka uongozi wa kanisa kumpa taarifa pale taratibu za ujenzi zitakapo anza ili mifuko hiyo iweze kuletwa.

Ukiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa kupita mbunge Ezra ametimiza ahadi hiyo ambayo kwa niaba yake imekabidhiwa na katibu wa mbunge Mashaka Maduka ambapo amesema kuwa wnanchi wanatakiwa kuwa na iaani na mbunge wao kwa kuwa ni mtu wakuishi ahadi zake na kuwa akiahidi anattekeleza.

PICHA: Naibu katibu mkuu wa UN atua Dodoma
Miaka 20 ya mashambulizi ya Septemba 11 Marekani