Tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2020 zimechelewa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababisha homa ya mapafu Covid 19 ambao ulisababisha kuzuia mikusanyiko.

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga wakati wa kuwaapisha majaji watakaozipitia kazi ziizowasilishwa kwaajili ya kushindanishwa.

“Jumla ya kazi 450 zimewasilishwa kushindanishwa katika makundi 21 ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2019”, amesema Kajubi.

Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya MCT, Jaji Mstaafu Juxon Mlay amewataka majaji hao kufanya kazi hiyo kwa uadilifu ili kuwe na ushindani utakaoleta tija katika tasnia ya uandishi wa habari.

Mamia ya waandamanaji wakamatwa Belarus
Kubenea mikononi mwa polisi