Baraza la Habari Tanzania (MCT), limeipongeza Serikali kwa kufanyia kazi kilio cha wadau cha siku nyingi cha kutaka kutungwa sheria ya kulinda data.

Taarifa ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji Taarifa kwa Wote (IDUAI), Septemba 28 ya kila mwaka, iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga, imeeleza kuwa lilitoa mwito wa kufanyiwa kazi ombi hilo la wadau la kutungwa sheria hiyo katika maadhimisho ya siku ya Haki ya Kujua mwaka jana.

Muswada wa sheria hiyo, ulisomwa Bungeni kwa mara ya kwanza Septemba 23, 2022 ambapo Mukajanga katika taarifa hiyo ameeleza kuwa, “ hii ni hatua kubwa ambayo inastahili kupongezwa.”

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Nchini, Kajubi Mukajanga.

Amesema, Serikali na wananchi wanatakiwa kuwa na uhakika kwamba Baraza na washirika wake watausoma muswada huo kwa umakini na kutoa mapendekezo yao kwa mujibu wa taratibu, ili hatimaye ipatikane sheria bora.

MCT, pia imehimiza kuchukuliwa hatua mbalimbali za kuimarisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi, kwa kuboresha taratibu za utoaji wa taarifa.

Siku ya Usafirishaji kutoa majibu hewa chafuzi, ajali
Serengeti Girls kuonja tamu, chungu za VAR