Wabunge watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga) na Saed Kubenea (Ubungo) jana wamesomewa rasmi maelezo ya awali ya tuhuma za kufanya shambulizi la kudhuru mwili.

Wabunge hao pamoja na diwani wa kata ya Saranga, Ephreim Kinyafu, diwani wa kata ya Kimanga, Manase Njema pamoja na mfanyabiashara Rafii Juma jana walisomewa maelezo hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka ya kumpiga na kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS), Theresia Mbando.

Wakili wa Serikali, Frola Massawe aliiambia mahakama hiyo kuwa Februari 27 mwaka huu washtakiwa hao kwa pamoja walimshambulia mlalamikaji katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alieleza kuwa walitekeleza tukio hilo katika ukumbi huo ambapo kulikuwa kulikuwa kukitarajiwa kukifanyika uchaguzi wa Meya na Naibu Meya.

Alisema kuwa walitekeleza kitendo hicho kwa pamoja baada ya kutoridhishwa na taarifa za kutokuwepo kwa uchaguzi huo iliyotolewa na mlalamikaji.

Wakili huyo wa upande wa Jamhuri alisema kuwa baada ya tukio hilo, Polisi waliendesha zoezi la utambuzi na ndipo mlalamikaji aliwatambua watuhumiwa hao kuwa ndio waliomshambulia.

Washtakiwa wote wanakana kutenda kosa hilo.

DC Mjema Kutatua kero za Wananchi kata za Mvuti na Msongole
Mtuhumiwa ugaidi akutwa amekufa mahabusu