Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Justine Maliwasa (CCM) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kuchoma moto msitu wa hifadhi ya Mbizi na kuisababishia Serikali hasara ya shilingi milioni 226.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema kuwa Maliwasa alikamatwa juzi baada ya watu waliokutwa wa kichoma msitu kudai ndiye aliyewatuma.

“(Maliwasa) anahojiwa baada ya watuhumiwa tuliowakamata kwa kosa la kuteketeza msitu huo wa hifadhi kwa moto walipodai kuwa wametumwa na Meya huyo (Maliwasa),” alisema Kamanda Kyando.

Msitu huo uliochomwa ni chanzo cha maji cha mji wa Sumbawanga kwa asilimia zaidi ya 80 na unasimamiwa na Mamlaka ya Huduma za Misitu (TFS).

Serikali: Muswada wa habari hausemi mwandishi ni mwenye shahada
Ole Sendeka amvaa Lowassa kwa kauli zake kuhusu hali ya maisha